Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

4/21/18

Makonda kupima tezi dume nyumba kwa nyumba


Wakati chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14 ikitarajiwa kuanza kutolewa Jumatatu wiki ijayo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ana mikakati ya kupita nyumba kwa nyumba ili kuwapima wanaume saratani tezi ya dume.


Makonda ameyasema hayo leo Aprili 21 wakati akifungua rasmi warsha ya chanjo hiyo iliyowashirikisha waandishi wa habari, wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali wa dini na siasa.


Amesema wakati saratani ya mlango wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba ambao hata hivyo hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo katika jamii. 


"Kuna kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu kuhakikisha hii kasi ya vifo kwa kinababa inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu," amesema Makonda. 


Pia, ametoa wito kwa viongozi wote wa serikali za mitaa na viongozi wa dini kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili wasichana wote wenye umri huo wafike kwenye vituo kwa wingi kupata chanjo.


Makonda amesisitiza pia kuzingatia kupata chanjo kamili kwa kurudi mara ya pili ili kuikamilisha.
Read More

Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 21, 2018


Read More

4/20/18

DPP alifunga jalada la kesi ya mauaji ya Akwilina

Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Biswalo Mganga amesema, jalada la kesi ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini amelifunga rasmi.

Hayo ameyasema leo Aprili 20, 2018; Ikulu jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari huku akionya watu wanaovunjua amani kutofumbiwa macho wakiwamo waandishi wa habari.

Amesema jeshi la polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano, haliwezi kushtakiwa au hata kukitokea vurugu na kusababisha mauaji huwezi kulishtaki jeshi.

”Katika maandamano yale ya watu zaidi ya 200, huwezi kubaini nani amehusika na kumpiga risasi Akwilina na mwili wake haukutolewa risasi yoyote.”

Alipoulizwa kuhusu askari waliokamatwa baada ya kutokea kwa tukio hilo, Biswalo amesema, “kama jalada nimelifunga, kwa hiyo askari wale nao wameachiwa huru hawana hatia.”

Mkurugenzi huyo amesema moja ya jukumu lake ni kuhakikisha amani inakuwapo,”na niseme tu kuwa, mimi sina chama cha siasa, si mwanasiasa, kwa hiyo sitamvumilia mtu awe mkubwa wala mdogo, nitamshughulikia.”

“Na wanaosema wataandamana, waambieni wasifanye hivyo kwani wakiandamana watakwenda kuwasilimulia familia yake,” amesisitiza Biswalo

Pia, amevionya vyombo vya habari ambavyo vinavyoweza kuchangia uvunjifu wa amani, hatua zitachukuliwa hivyo kuvitaka kuwa makini na kutimiza wajibu wao kwa kufuata misingi ya taaluma yao.
Read More

Jafo apiga marufuku uchimbaji wa mchanga kwenye mito ya Dar es salaamWaziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo (Mb) amepiga marufuku uchimbaji wa mchanga unaoendelea katika mito mbalimbali Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Jafo alitoa katazo hilo wakati wa ziara yake ya kuangalia athari zilizotokana na mafuriko ambapo katika barabara za mwendokasi eneo la Jangwani na Manispaa ya Ilala leo tarehe 20 Aprili 2018.

Akiwa katika kata ya Gongolamboto eneo la Ulongoni A na Ulongoni B, alijionea jinsi ambavyo mafuriko yaliyotokana na wingi wa mvua zilizonyesha yalivyoharibu madaraja na kuacha athari kubwa kwa wananchi.

“Nimejionea mwenyewe jinsi ambavyo mvua hizi zimeleta athari kubwa hapa na kusababisha mawasiliano kukatika baina yenu nyinyi na wenzenu wa upande wa pili. Lakini niwaambie kuwa kwa sehemu kubwa baadhi ya wananchi wanachangia uharibifu wa maeneo haya kutokana na uchimbaji wa mchanga unaoendelea na kusababisha uharibufu katika kingo za mito pamoja na miundombinu hii iliyojengwa,” alieleza Mhe. Jafo

“Hatuwezi kuzizuia mvua zisinyeshe lakini hatuwezi kuvumilia kuwaacha watu wanaoharibu miundombinu na kingo za mto kwa kuchimba mchanga. Hivyo kuanzia leo napiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika maeneo yote ya mito ya Dar es Salaam,” aliagiza Waziri Jafo.

Waziri aliendelea kueleza kuwa miundombinu inajengwa kwa gharama kubwa na Serikali lakini wapo watu ambao wanaiharibu kwa makusudi kutokana na uchimbaji wa mchanga, hivyo akaeleza kuwa Serikali haitavumilia swala hilo.

Alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sofia Mjema aliyeambatana naye katika ziara hiyo kusimamia agizo hilo pamoja Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla wake, na akaagiza kuwakamata wale wote watakaokaidi agizo hilo.

Aidha Mhe. Jafo alieleza kuwa Serikali inajitahidi kurejesha mawasiliano katika maeneo hayo yaliyoathirika kwa kujenga madaraja ya muda wakati wakisubiri ukarabati mkubwa kufanyika.

Alieleza kuwa amewasiliana na Waziri wa Ulinzi Mhe. Hussein Mwinyi ili Jeshi la Ulinzi lisaidie katika kutengeneza madaraja hayo.

“Waziri wa Ulinzi ameniahidi kuwa anatuma wataalamu wa Jeshi kufanya tathmini ya uharifu ili kutengeneza madaraja hayo ya muda,” alisema Jafo.

Awali, katika ziara hiyo Mhe. Jafo alitembelea Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi “DART” katika kituo cha Jangwani na kuangalia athari zilizoltokana na mafuriko.

Akiwa katika kituo hicho cha Jangwani alipongeza uongozi wa UDART kwa kuzingatia agizo lake alilolitoa awali la kuyahamisha mabasi katika kituo hicho na kuyalaza Kimara pamoja na Gerezani hivyo kufanikiwa kuokoa mabasi hayo.

“Mmeniambia kuwa yale mabasi niliyoyaona hapa wakati wa mafuriko ni yale ambayo yalikuwa hayatembei kabisa na hata hivyo mmetoa vifaa amabavyo vingeharibika katika mabasi hayo na mengine yote mliyatoa hapa. Nawapongeza kwa hilo,” alieleza Jafo.

Mhe.Jafo alisema kuwa mafuriko hutoke duniani kote marekani, china na kwingineko na hatuwezi kuyazuia, lakini ni akasema kuwa ni lazima wadau na wananchi wote wazingatie tahadhari zinazotolewa ikiwa ni pamoja na kuhama mabondeni ili kupunguza athari.

Pia alieleza kuwa Serikali inampango mkubwa wa kuutengeneza Mto Msimbazi kupitia Mradi wa DMDP, ambapo takribani dola za kimarekani 20 milioni zimetengwa ili kupata suluhisho la kudumu. Alieleza kuwa kazi hiyo inatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2018 mara baada ya kumalizika kwa usanifu.
Read More

Tanzia: Mrembo Agness Masogange Amefariki Dunia


Mwanamitindo na video queen marufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia jioni ya leo April 20 alipokuwa amelazwa katika hospital ya Mama Ngoma akipatiwa matibabu

Akithibitisha taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.

Tayari mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.

Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.

Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017.
Read More

Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 20, 2018


Read More

4/19/18

Yanga Yatua kwa Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia.
Kikosi cha Yanga kimeanza safari ya kutoka Hawassa kuelekea jijini Addis Ababa ambapo mchana wa leo kitakula chakula cha pamoja na balozi wa Tanzania nchini Etgiopia.


Yanga jana jioni ilikata tiketi ya kushiriki hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kuwaondoa Welayta Dicha kwa jumla ya mabao 2-1 licha ya mchezo ya kupokea kipigo cha bao moja kinakwenda kwa balozi kufuatia mualiko maalum.


Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hamad Islam ameondoka na timu hiyo asubuhi Hawassa amesema wamepokea simu kutoka kwa balozi akiitaka timu hiyo kufika nyumbani kwake kuwapa mkono wa pongezi.


Islam alisema ikiwa hapo Yanga itapata chakula cha mchana na kuagana na balozi kabla ya kuanza safari ya kurudi nyumbani wakipitia Kenya na kutua jijini Dar es Salaam saa saba usiku.


"Mheshimiwa balozi ametuita kwake kutupa mkono wa pongezi baada ya mafanikio ya jana, unajua hakupata nafasi ya kuja uwanjani, lakini sasa amesema angalau akawapongeze vijana pale kwake," alisema Islam.


"Tukiwa pale ataongea na vijana kidogo lakini ilikuwa tuate chakula hapa Hawassa ametuzuia akitaka tupate chakula hicho tukiwa naye tukimaliza hapo jioni tutaanza safari ya kurudi nyumbani tukipitia Kenya na tunataraji kufika nyumbani Tanzania saa saba usiku."
Read More

Meneja wa TPA Afikishwa Mahakamani kwa Kumiliki Nyumba 23, Magari 7

Leo April 19, 2018 Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Prosper Kimaro amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.4 zisizolingana na kipato chake halali.

Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Bilioni 1,178,370,334, zilizopo maeneo ya Temeke DSM na magari 7 yenye thamani Shilingi Milioni 307,364,678.20.

Kimaro amesomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.

Wakili Vitalis amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa amelitenda kosa hilo kwa miaka tofauti kati ya 2012 na 2016.

Anadaiwa mali hizo amejilimbikizia maeneo ya Temeke DSM akiwa mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa na mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na cha sasa.

Mali hizo ni nyumba 2 zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke (Mil 124.2), kiwanja kimoja kilichopo Yombo Vituka (Mil.12.9), nyumba 2 zilizopo Temeke (Mil 63.5).

Pia nyumba nyingine 3 zilizopo Temeke zenye thamani ya (Mil.159), nyumba nyingine 3 zilizopo maeneo hayo (Mil 170.1), nyumba nyingine moja (Mil 71.3).

Pia ana kiwanja Temeke (Mil 35), kiwanja kingine (Mil 25) na kujenga nyumba 3 (Mil 159), pia nyumba nyingine moja (Mil 106), pia nyumba nyingine 3 zilizopo Temeke zikiwa na thamani ya (Mil 214).

Pia ana nyumba 4 zilizopo Viziwa Ziwa Kibaha Mjini (Mil 199.7), nyumba nyingine Kilimahewa Tandika (Mil 70).

Pia anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise (Mil 180.1), Mitsubishi (Mil 38.4), Massey Ferguson (Mil.24), Trailer (Mil 4.5), Toyota Harrier (Mil 35.8), Trailer (Mil 4.8), Massey Ferguson (Mil 19.1).

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana makosa yake ambapo Wakili Vitalis amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hana pingamizi na dhamana.

Hakimu Simba ametoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini 2 watakaowasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.Mil 200, pia mshtakiwa asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali pamoja na kuwasilisha hati zake za kisafiria.

Mshtakiwa huyo hajatimiza masharti ya dhamana, ambapo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 3,2018.

#millardayo
Read More