Ratiba ya Leo Jumapili Ligi Kuu Tanzania Bara | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

1/21/18

Ratiba ya Leo Jumapili Ligi Kuu Tanzania Bara


Baada ya michezo mitatu ya ligi kuu VPL mzunguko wa 14 kupigwa kati ya juzi na jana, ligi Tanzania Bara itaendelea leo kwa michezo mitatu itakayopigwa katika viwanja tofauti.


Michezo mgumu unatajwa kuwa kati ya Tanzania Prisons watakaowakaribisha Azam Fc katika dimba la Sokoine-Mbeya kuanzia majira ya saa 16:00 jioni.


Michezo wa pili nao pia utakuwa mgumu, baada ya kutopata matokeo mazuri katika mechi 3 mfululizo mabingwa watetezi wa ligi VPl, Young Africans watakuwa wageni wa maafande wa Ruvu Shooting katika dimba la Taifa Jijini Dar es salaam, kuanzia majira ya saa 16:00 jioni.

Na mchezo wa mwisho utazikutanisha Ndanda Fc watakaokuwa wageni wa Mwadui Fc katika dimba la Mwadui Complex-Shinyanga majira ya saa 16:00 jioni.

MAGOLI 4 YA SIMBA DHIDI YA SINGIDA UNITED 18/01/2018
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin