Sugu na mwezake wafikishwa mahakamani leo | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

1/22/18

Sugu na mwezake wafikishwa mahakamani leo


Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ leo Junuari 22. 2018 amefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kusikiliza kesi inayomkabili ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.


Sugu pamoja Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga walifikishwa mahakamani hapo Januari 19, 2018 lakini mahakama ilizuia dhamana zao na kuwarejesha rumande hadi leo.

Siku hiyo hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Michael Mteite alitoa uamuzi wa kuwarejesha rumande, kwamba kesi hiyo inatakiwa isikilizwe mfululizo kwa muda mfupi na washtakiwa wakiwa wanafika mahakamani hapo wakitokea mahabusu.

Sugu na mwenzake wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli ambayo waliyatoa katika mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin