Bil. 1.2 Kukarabati Shule ya Sekondari Kondoa | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

2/11/18

Bil. 1.2 Kukarabati Shule ya Sekondari Kondoa


Kaimu Mkurugenzi wa Malmaka ya Elimu Tanzania Bi Graceana Shirima (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Mji Kondoa Khalifa Kondo orodha ya vifaa kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Wasichana Kondoa.


Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imekabidhi jumla ya Bil 1.2 kwa ajili ya Ukarabati wa Shule ya Sekondari ya Waschana ya Kondoa.

Akikabidhi fedha hizo Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema kuwa, majengo ambayo yatakarabatiwa na fedha hizo zinazo fikia bilioni 1.2 ni pamoja na mabweni, jiko na bwalo, jengo la utawa, maktaba, zahanati na vyoo.

“Tuna imani na uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa na Bodi ya Shule hawatatuangusha katika usimamizi na watatumia fedha hizi kama ilivyo elekezwa”, alisema Shirima na kuwashauri kuwatumia mafundi wenyeji na pia kuwataka kutumia utaratibu wa “force account” ili kurahisisha na upatikanajiwa vifaa vya ujenzi kwa gharama nafuu.

Shirima aliongeza kuwa lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha shule inakuwa na mazingira bora ya kujifunza na kujifunzia

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mhe. Hamza Mafita alisema wanaishukuru serikali kwa kuimbuka shule ya hiyo kwa kuwaletea fedha hizo ambazo kutokana na maelekezo yaliyotolewa zitawezesha uchumi wa wananchi wa kondoa kunufaika.

Akingea wakati wa hafla hiyo ya Makabidhiano, Mkurugenzi wa Mji wa Kondoa Khalifa Kondo, alisema imekuwa ni neema ya pekee kwa Halmashauri hiyo kwani imesaidia kuokoa fedha za Halmashauri zilizopangwa kutumika kukarabati shule hiyo.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin