Uhamiaji Watoa Majina na Picha za Watumishi wake Waliofukuzwa Kazi ili Kuwatahadhalisha Wananchi | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

2/16/18

Uhamiaji Watoa Majina na Picha za Watumishi wake Waliofukuzwa Kazi ili Kuwatahadhalisha Wananchi


Idara ya Uhamiaji imewatahadharisha wananchi kuwa makini na watumishi wake walioacha kazi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufukuzwa kati ya mwaka 2016 na 2017 ili kuepuka kutapeliwa.
Akizungumza jana, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt Anna Makakala alisema kuwa wametoa tahadhari hiyo ili kuwanusuru wananchi kutapeliwa kutokana na baadhi ya watumishi hao waliofukuzwa kurndelea kujifanya ni watumishi wa Idara hiyo huku wakitaka kutoa huduma kwa wananchi.
Alisema kuwa Idara imeamua kuwatangaza hadharani ili wananchi wawatambue, na kuwataka wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi watakapowaona watu hao wakijihusisha na shughuli za Idara ya uhamiaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
Watumishi hao ni Thobias Lyewe, Julieth Mrema, Nina Mliga, Loveness Wilson, Wilbard Ompapson, Salama Dilunga, Philbert Chaula, Mkombozi Chodri na Alfred Mrema.
Wengine ni Imakulata Mwakatika, Ramadhani Ally, Ritha Maganga, Jovin Mkuchu, Veronika Max, Angela Mwambwiga, Peter Bally, Elizabeth Kibinga, na Lucy Munyanga.
Kwa upande wake, Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ally Mtanda alieleza kuwa kumekuwa na watumishi ambao tayari wameachshwa kazi lakini bado wanatumia kivuli cha idara hiyo kuwarubuni watu mbalimbali na kuwadanganya kuwa wao ni watumishi halali.
“Kuna shida inatokea kwa watu wengi kujitambulisha kuwa wanatoka Uhamiaji. Wanakwenda viwandani na maeneo mengine kisha kuwarubuni watu na kuchukua fedha,” alisema Mtanda.
“Wale kwa namna moja au nyingine walifuzwa kazi na wengine wameacha wenyewe kazi lakini wanaendelea kujitambulisha ndiyo maana tumeamua kuitoa orodha hii ili wananchi wawatambue kwamba hawa si watumishi wetu na hatutahusika kwa lolote likitokea,” alisisitiza.
Hapa chini ni picha pamoja na majina ya watumishi hao waliofukuzwa kazi.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin