Baada ya Kufutiwa Kifungo na Waziri Roma Atangaza Kuufuta Wimbo wa “Kibamia” | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/30/18

Baada ya Kufutiwa Kifungo na Waziri Roma Atangaza Kuufuta Wimbo wa “Kibamia”Waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo Dkt Harrison Mwakyembe akiambatana na Naibu waziri Juliana Shonza, katibu mtendaji wa BASATA Geofrey Mngeleza, Mwakilishi wa bodi ya filamu Tanzania na Katibu wa chama cha muziki wa kizazi kipya wameamua kukutana na wasanii ambao ni Roma Mkatoliki na Pretty Kind

Moja kati ya vitu ambavyo wamejadili ni maombi yao ya kusamehewa adhabu zao za kufungiwa na kujishugulisha kwenye sanaa ya muziki kwa kipindi cha miezi sita kwa upande wa Roma baada ya kutangaza kusamehewa alitangaza kuufuta wimbo wake wa “Kibamia” .

Roma Mkatoliki alisema……..>>>“Mimi kama Roma au kama mtu niliotoa bidhaa kuna maamuzi ambayo tumefikia ni kwamba ile bidhaa ina ukakasi na mimi nasema kama mwenye bidhaa vyombo ama mamlaka na taasisi ambazo zinasimamia hizi bidhaa kuingia sokoni ziweze kuiondoa hiyo bidhaa mara moja”
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin