Belle 9 Awashangaa BASATA, Awafananisha na baba asiyejua jina la mtoto wake | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/1/18

Belle 9 Awashangaa BASATA, Awafananisha na baba asiyejua jina la mtoto wake

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Belle 9 amelishangaa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa kushindwa hata kuwajua wasanii japo hata kwa majina.

Belle 9
Belle 9 amesema hayo baada ya BASATA kuchanganya majina kwa kumtaja kwenye orodha ya wasanii waliofungiwa nyimbo zao jana Februari 28, 2018 badala ya kuweka jina la Roma Mkatoliki.
Kwahiyo mimi ni Roma Mkatoliki haya basi tongwe record baby jei mada yo yo yo Roma!  Hii ni sawa na kua na baba ambaye akisikia umekosa ana kuhukumu lakini akiulizwa jina la mwanao anaitwa nani anajiuma uma halafu analitaja jina la mtoto wa jirani ambalo huwa analiskia akiwa anakuja kukuhukumu,“ameandika Belle 9 kwenye ukurasa wake wa Instagram.
BASATA walikosea kumtaja Belle 9 kwenye kipengele cha wimbo wa Kibamia ambapo waliandika Abemego Damiani a.k.a Roma Mkatoliki.

Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin