Hii ndiyo U-Tube aliyomaanisha Waziri Jafo | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/7/18

Hii ndiyo U-Tube aliyomaanisha Waziri Jafo
Asubuhi ya leo March 7, 2018 imesbaa video ambayo ilikuwa ni kipande cha mahojiano baina ya mtangazaji wa kituo kimoja na television na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo katika kipindi TV hiyo na video hiyo kuleta gumzo mtandaoni.

Waziri Jafo kwenye mahojiano hayo alitaja kifaa kinachopatikana maabara kinachoitwa U-tube na kusambaa kwa video hiyo kulitokana na watu kuhisi Waziri Jafoamekosea na amemaanisha mtandao wa YouTube na ndipo suala hilo lilipozua mijadala.

Kutokana na hilo Waziri Jafo amefafanua kuwa hakukosea kusema neno hilo la U-tube, bali alimaanisha kifaa kinachotumika maabara kipindi akifafanua jinsi shule kongwe nchini zilivyo kwenye hali mbaya ya mpaka Serikali ya awamu ya Tano kuamua kuzifanyia ukarabati.

“Hapo awali shule hizo unaweza ukakuta vifaa vya maabara ni chakavu, mfano Bunsen Burner na U-tube iliyokuwa inatumika miaka ya 80 zimechakaa mpaka kupoteza ubora wake lakini bado zinatumika mpaka sasa. Ndio maana serikali imeamua kuboresha shule hizo kongwe ili ziweze kurudi katika ubora wake.” – Waziri Jafo.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin