STAMINA: Tulipewa Miezi 6 Kubadili "KIBAMIA" , Ashangaa Kufungiwa Kwa ROMA huku Muda Waliopewa Ukiwa Haujaisha. | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/2/18

STAMINA: Tulipewa Miezi 6 Kubadili "KIBAMIA" , Ashangaa Kufungiwa Kwa ROMA huku Muda Waliopewa Ukiwa Haujaisha.

RAPA Stamina ambaye anaunda Kundi la ROSTAM na rapa mwenzake Roma Mkatoliki, ameonyesha kushangazwa na maamuzi ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kumfungia Roma jana Alhamisi, Machi 1, 2018.

Stamina amesema hayo baada ya Roma kufungiwa kujihusisha na sanaa ya muziki kwa kutofanya marekebisho ya maudhui katika wimbo wao wa Kibamia walimshirikisha Maua Sama.

“Kibamia ilitoka Novemba 22, 2017, mimi na Roma Roma Mkatoliki tuliitwa BASATA Desemba 6, 2017 na Waziri akasema wametupa miezi sita kufanya marekebsho, leo ndio kwanza Machi 1, 2018, mbona miezi sita bado? Au miezi sita ya Tanzania iko tofauti na kalenda ya dunia nzima? Mna tatizo gani na wasanii wetu BASATA na Wizara? Mnakuza au mnauwa sanaa?” alihoji Stamina.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin