Taharuki sauti mlipuko mahakama ikiendelea Dar | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/2/18

Taharuki sauti mlipuko mahakama ikiendelea Dar


Image result for taharuki ya mlipuko mahakamani
JENGO la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, jana lilinusurika kuteketea kwa moto kutokana mlipuko uliotokana na hitilafu ya umeme.


Sauti ya mlipuko ilisababisha taharuki kubwa kwa askari wa Jeshi la Polisi na Magereza ambao walilazimika kutumia vifaa vya kuzimia moto kuzima mlipuko huo.

Mlipuko huo ulitokea saa nne asubuhi wakati watumishi wa mahakama hiyo wakiendelea na shughuli zao pamoja na wananchi waliofika kusikiliza kesi zao wakiwa katika viunga vya mahakama kuingiwa na woga kutokana na tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya jengo hilo, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mkoa wa Dar es Salaam, Gasto Kanyairika, alisema hitilafu hiyo iliathiri utendaji wa kazi kutokana na shughuli zote zinazotegemea umeme kusimama.

“Huduma za mawasiliano ya Shirika la Simu Tanzania (TTCL) tunazotumia katika jengo hili na kwenda nje ya jengo na huduma za mtandao kupitia Kampuni ya Halotel zote zimeungua, hakuna mawasiliano... Kama mnavyooana giza limetawala katika jengo hili na baadhi ya watumishi wako nje ya ofisi zao,” alisema na kuongeza:

“Askari wetu walifanikiwa kuzima moto kabla ya kusambaa na vyombo vya uchunguzi vimefika likiwamo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wameshaangalia, tunasubiri wafanye kazi yao ili kumaliza tatizo,” alisema Kanyairika.

Akizungimzia kuhusu hasara iliyopatikana, alisema wataalamu wao wa Tehama walifika na walikuwa wanasubiri uchunguzi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (Temesa) ili kubaini hasara iliyosababishwa na hitilafu hiyo.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin