Uzinduzi Wa Duka Jipya TECNO-EXPERIENCE CENTER Samora | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/25/18

Uzinduzi Wa Duka Jipya TECNO-EXPERIENCE CENTER Samora


Kampuni ya simu za mkononi, TECNO inayofanya kazi chini ya TRANSSION HOLDINGs imezidi kutanuwa wigo  wa soko la simu nchini kwa kufungua duka jipya maarufu  “Experience Center’’ Dar es salaam, Samora, jumamosi 24/03/2018, uzinduzi huo ulihudhuriwa na naibu waziri mawasiliano na uchukuzi mheshimiwaAtashasta Nditiye,  watu maarufu, wageni waalikwa, wadau wa TECNO kutoka mtandaoni na nyanja mbalimbali nchini.
Mgeni rasmi Naibu waziri mawasiliano na uchukuzi Mheshimiwa Atashasta Nditiye alishiriki zoezi la kukata utepe pamoja na mkurugenzi mkuu wa TECNO Bwana Xu pamoja na meneja wa Clouds media group Ruge Mutahaba
Mheshimiwa pia aliweza kuzunguka sehemu mbalimbali za duka hilo kujionea huduma mbalimbali zinazopatikana, ni wazi TECNO imekua chachu ya kukuza Teknolojia na mawasiliano ambapo asilimia 94 ya wananchi wana mawasiliano nchini, lakini mapongeza kitendo cha watumiaji kupewa elimu ya namna ya kutumia simu janja kuepuka uhalifu, nawapongeza sana TECNO"alisema Naibu waziri Nditiye.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa TECNO nchini, Daniel Xu alisema “Ni furaha kujumuika nanyi katika uzinduzi wa duka la TECNO “Experience Center”, wateja watapata fursa ya kununua bidhaa, kupewa elimu ya bure kuhusiana na matumizi,sifa na mifumo mbalimbali ya simu, lakini pia huduma ya matengezo “after sales service” kupatikana papo hapo dukani. 

Uzinduzi huu unatoa fursa nyingine ya ajira kwa vijana wa kitanzania ili kuwainua kiuchumi, ambapo zaidi ya vijana 500 wa kitanzania wameshaajiliwa kwenye kampuni ya TECNO, Mkurugenzi Xu alimaliza.

Pia sherehe hzio zilipata ugeni kutokakwa wanamuziki na mastaa tofauti tofauti ikiwemo mchekeshaji almaarufu kama Jay Mondy, ambapo alijuimika na wadau wa TECNOkupitia kurasa zake za mtandaoni. Kulikua na michezo, elimu na burudani kabambe na bahati nasibu.
Naibu waziri Nditiye akiendesha zoezi la bahati nasibu,na baadayealikabidhi zawadi kwa wateja waliojishindia zawadi kabambe kupitia droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa kwa hisani ya TECNO.
Naibu waziri Mh. A. Nditiye, Mkurugenzi wa TECNO na meneja masoko Franck Luo, wakiwa na baadhi ya washindi wa bahati nasibu.

Kampuni ya TECNO inawakaribisha katika duka lao jipya linalopatikana Samora, Posta
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin