Watanzania kushuhudia Kombe la Dunia | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

3/1/18

Watanzania kushuhudia Kombe la Dunia

Image result for Pamela Kikuli
TIMU ya soka ya Tanzania itakayoshiriki mashindano ya maalumu yatakayojulikana kwa jina la ‘Castle Lager Africa 5s’ , itapata nafasi ya kwenda kushudia fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Juni mwaka huu, imeelezwa.


Mashindano hayo yenye hadhi ya kimataifa yatashirikisha timu za wachezaji watano (5) kila upande, na kocha mmoja na mechi zake zitakuwa zikichezwa kwa dakika saba ili kupata mshindi.

Akizungumza jana, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, alisema kuwa mchakato wa kupata timu itakayopeperusha bendera ya Tanzania utafanyika kwa kupitia katika baa mbalimbali hapa jijini Dar es Salaam.

Kikuli alisema kuwa bingwa wa michuano hiyo hapa nchini atafuzu kwenda kushiriki katika mashindano ya kimataifa pamoja na timu nyingine tano ambazo ni Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland na Lesotho.

"Mshindi atapata fursa ya kwenda Urusi kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia akiwa ameambatana na mashabiki wawili ambao watapatikana katika mchakato malumu pamoja na mchezaji mmoja mkongwe kutoka nchi ambayo itakuwa bingwa," alisema Kikuli.

Aliongeza kuwa endapo Tanzania itafanikiwa kushinda katika mashindano hayo, timu hiyo pamoja na mashabiki hao wawili wataongozana na mkongwe wa hapa nchini, Ivo Mapunda, ambaye aliwahi kuidakia timu ya Taifa (Taifa Stars), Yanga na Simba.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin