Ajali Mbaya Yatokea Tabora, Fuso na Basi la City Boy Zagongana Uso kwa Uso | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

4/5/18

Ajali Mbaya Yatokea Tabora, Fuso na Basi la City Boy Zagongana Uso kwa Uso

Watu kadhaa wamefariki dunia baada ya basi la abiria la City Boys lililokuwa likitokea Karagwe kwenda Dar es Salaam, kugongana uso na fuso katika eneo la Igunga Mkoa wa Tabora usiku wa kuamkia leo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema yupo njiani anaelekea katika eneo ilipotokea ajali hiyo kwa ajili ya kupata taarifa zaidi.
 
Alipoulizwa kuhusu idadi ya vifo na majeruhi vilivyotokana na ajali hiyo Kamanda Mutafungwa amesema atatoa taarifa rasmi kuhusu idadi ya vifo na majeruhi wa ajali hiyo atakapofika eneo la tukio.
 
Inaelezwa kuwa idadi kubwa ya abiria waliokuwa kwenye basi wamefariki dunia.(idadi kamili bado haijafahamika)
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin