Michezo: Waziri Ummy ajitosa usajili Coastal Union | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

4/15/18

Michezo: Waziri Ummy ajitosa usajili Coastal UnionBAADA ya kuhakikisha timu yake ya nyumbani, Coastal Union imerejea Ligi Kuu Tanzania Bara, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, amesema anahitaji kuona ushirikiano unaendelea ili kuhakikisha wanasajili wachezaji watakaoisaidia timu hiyo kupambana katika msimu ujao.


Waziri Ummy aliliambia gazeti hili kuwa umoja waliokuwa nao wakiundeleza, Coastal Union itarejesha makali yake na haitakuwa timu ya kupanda na kushuka daraja kila mara.

Alisema anaamini umefika wakati wakazi ya jijini Tanga "kuzika" tofauti zao na kuhakikisha wanaichangia timu yao kwa kila hali ili kufikia malengo.

"Ni kweli mimi ni shabiki wa Simba ambaye niko kamili katika masuala mbalimbali, lakini nikiwa Tanga nataka kuona Coastal Union inakuwa na makali na heshima yake tuliyoizoea na kuikuta wakati ninakuwa," alisema Waziri huyo.

Aliongeza kuwa mbali na kusaidia hamasa katika mkoa wao, pia kuwapo kwa timu hiyo kutasaidia kuinua kipato cha uchumi pale timu itakapokuwa inacheza nyumbani.

Mbali na Coastal Union, timu nyingine zilizopanda daraja ni pamoja na JKT Tanzania, Alliance School, KMC, Biashara United na African Lyon
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin