NMB yajitolea kuboresha sekta ya elimu | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

5/9/18

NMB yajitolea kuboresha sekta ya elimu


KATIKA kuboresha huduma ya elimu na kuongeza ubora katika sekta hiyo benki ya NMB imekabidhi vifaa vya shule vyenye thamani ya Sh. milioni 25 katika shule za msingi na sekondari zilizopo wilayani Tarime Mkoa wa Mara. 


Meneja wa Kanda ya Ziwa, Benki ya NMB, Abraham Augustino. 

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda ya Ziwa, Benki ya NMB, Abraham Augustino kwenye risala ya ufunguzi wa tawi jipya Wilaya ya Sirari. 

“Kila mwaka benki hutenga asilimia moja ya faida yake baada ya kodi kwa ajili ya kutoa msaada kwenye huduma za jamii hasa kwenye sekta ya afya, elimu, majanga na mambo mbalimbali,” alisema Augustino . 

Augustino aliongeza kuwa shule za msingi tatu zilizopo wametoa madawati 100 yenye thamani ya Sh. milioni 10. 

Kwa upande wake, Glorious Luoga ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime aliyekuwa mgeni rasmi, aliishukuru benki hiyo kwa kuona changamoto hizo. 

Aliwataka wananchi kuchangamkia uwepo wa benki hiyo kuwa karibu yao na kuitumia kukuza uchumi na ajira, ili kujipatia maendeleo yao. 

" Serikali ya awamu ya tano imeweka mikakati mizuri ya kupunguza umaskini kwa wananchi wake hivyo nao wachangamkie fursa zote za kibenki zinazojitokeza mbele yao hasa za mikopo,” alisema .
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin