Watumishi Wapya 26 wafukuzwa kwa vyeti feki | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

5/1/18

Watumishi Wapya 26 wafukuzwa kwa vyeti feki


Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala mkoani Mtwara limeridhia kuwafukuza kazi watumishi wake 26 kutokana na tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo udanganyifu pamoja na utoro kazini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Newala, mkoani Mtwara, Rashid Ndembo na kuongeza kuwa watumishi hao wamefukuzwa kazi baada ya kubainika kuwa wameleta vyeti vya udanganyifu pamoja na kutoroka kazini.

“Kuna watumishi wengine 12 kati ya hao 26 nao tumewafukuza kazi kwa sababu ya utoro kazini. Kwa maana kwamba baada ya baadhi yao kugundua kwamba walikuwa wameleta vyeti vya udanganyifu wakaamua kujiondoa wenyewe. Walipokimbia wengine wakaonekana wamemdanganya Waziri kwa kuleta vyeti feki na la pili utoro kazini,” alisema Rashid Ndembo.

Ndembo amewataja watumishi hao luwa ni walimu pamoja na watumishi wengine wa kawaida ambapo miongoni mwao 14 wamefukuzwa kwa udanganyifu wa vyeti na 12 kutokana na utoro kazini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo ametumia nafasi hiyo kulipongeza Baraza la Madiwani kwa uamuzi wao wa kuwachukulia hatua watumishi hao na kueleza kuwa anawaunga mkono kwa nia ya kuleta maendeleo.“Kwa hatua ambazo mmezichukua kwa kuwachukulia hatua watumishi wa namna hiyo, mimi niwapongeze sana na niko pamoja na ninyi. Wala silalamiki. Nasema kaza buti,” alisema Mkuu wa Wilaya ya Newala.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin