HELSB NA ZHELB ZATOA MAELEKEZO KWA WANAFUNZI WAPYA WA ELIMU YA JUU 2018/2019 | Yuvinusm-Habari Unazozitaka
Breaking News
Loading...

8/12/18

HELSB NA ZHELB ZATOA MAELEKEZO KWA WANAFUNZI WAPYA WA ELIMU YA JUU 2018/2019
Waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wanafunzi waliofaulu katika mitihani yao ya kidato cha sita kuhakikisha kuwa wanakwenda kusoma fani ambazo serikali inazihitaji.

Waziri Wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma amewataka wanafunzi waliofaulu katika mitihani yao ya kidato cha sita kuhakikisha kuwa wanakwenda kusoma fani ambazo serikali inazihitaji.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika semina ya kuwaelimisha wanafunzi hao juu ya kuchagua fani ambazo serikali inazipa kipaumbele katika Skuli ya Haile Salasi, Mhe. Waziri alisema kuwa katika hatua walioifikia wanafunzi hao uwezo na vibaji vyao ndipo vitakapo onekana. Hivyo basi, aliwataka huko wanakokwenda waweze kupambana ili kupata ufanisi wa masomo yao.

Aliongeza kuwa Serikali inahitaji wataalamu kutoka fani tofauti kulingana na vipaumbele vilivyopo kama vile fani za mafuta na gesi, Afya, Kilimo, Madaktari wa wanyama n.k. kwani fani hizo zinahitaji wataalamu katika nchi yetu.

Sambamba na hayo Mhe, Waziri aliwashukuru wahitimu hao kwa kupata matokeo mazuri ya mitihani yao na kuitikia wito kwa kufika katika semina hiyo.

Aidha, alizishukuru Bodi za Mikopo za Elimu ya juu Zanzibar na Tanzania Bara kwa kuamua kwa makusudi kuwaita wanafunzi hao ili kuwapatia uelewa juu ya masuala mazima ya mikopo kupitia taasisi hizo.

Nae Mkurugenzi Tume ya Mipango Zanzibar Bi Salama Makame aliomba wanafuzi hao waangalie vipaumbele wakati wa kuchagua masomo ambayo serikali inahitaji wataalamu hao.

Pia aliwataka kuhakikisha kuwa uzalendo wanauweka mbele baada ya kumaliza masomo yao ni vizuri kurejea nyumbani kwani serikali imegharamika kwa kiasi kikubwa kwa ajili yao, hivyo basi nao wanahitaji kurejesha shukurani hizo.
Weka Maoni yako Hapa

google+

linkedin